MKUFU WA LIL WAYNE WAMSAIDIA KULIPA ADA

LONDON, England


MWANAFUNZI wa sanaa ambaye alitengeneza mkufu wa dhahabu kwa rapa nguli, Lil Wayne, amesema mauzo yake yalimsaidia kulipa karo yake ya chuo kikuu.

Joy Bonfield-Colombara, 29, kutoka Kusini Mashariki mwa Jiji la London, alisema alikuwa na wakati mgumu kulipa karo ya pauni 9,500 kwa mwaka kwenye Chuo cha Sanaa cha Royal College of Art.

Hata hivyo, alisema juzi kwamba wakati akitathmini kuacha masomo, alipata ujumbe wa barua pepe kutoka kwa rafiki wa rapa huyo raia wa Marekani, ambaye alikuwa anataka kumnunulia mkufu huo kama zawadi ya siku ya kuzaliwa.

 

Bonfield-Colombara, ambaye pia anafahamika kama Joy BC, alisema kwamba alishangaa sana wakati alipojulishwa kiwango cha fedha ambacho angelipwa alichosema ni maelfu kadhaa wa pauni.

Alisema alikuwa na muda wa wiki mbili hadi tatu kumaliza kazi hiyo kabla ya siku ya kuzaliwa ya miaka 36 ya Lil Wayne.

“Nilimpigia mpenzi wangu simu na kumwambia nimeshangazwa sana,” alisema.

“Nilichonga kila kitu kwa mikono yangu, hunichukua muda mrefu sana. Mkufu mmoja nilimtengenezea mtu ulinichukua miezi 9.

“Mpenzi wangu aliniambia nisitengeneze sawa na wa Ronaldo,” alisema. Akimaanisa sanamu ya Ronaldo iliyokosolewa sana kwenye mitandao ya kijamii.

Bonfield-Colombara ambaye aliwahi kusomea Glasgow School of Art, alisema amekuwa akituma maombi ya msaada kwa masomo yake.

“Mama yangu alichukua mkopo wa benki na mimi nikapata mkono wa Serikali, kwa mahitaji yangu nilitegemea karo yangu.”

“Nilihitajika kutafuta karibu pauni 10,000. Nilitumia mtandao wa GoFundMe nikafanikiwa kuchangisha pauni 1,500, kisha nikapata barua pepe hii.”

“Licha ya fedha nilizopata kwa mkufu huu haziwezi kulipa karo yangu yote, zinalipa sehemu kubwa.”


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*