MISS TANZANIA KUWEKA HISTORIA KESHO DAR

 

 

NA MWANDISHI WETU


TASNIA ya urembo nchini inatarajia kushuhudia mapinduzi mapya ya shindano la Miss Tanzania kesho katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, Posta, Dar es Salaam, baada ya kufanyika mabadiliko makubwa.

Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basila Mwanukuzi, ameliambia Papaso la Burudani kuwa maandalizi yamekamilika tayari kwa wadau wa tasnia kushuhudia mrembo mpya atakayekabidhiwa taji la Miss Tanzania na Diana Edward, Miss Tanzania 2016/17.

“Watu wajitokeze na kuona namna tutakavyompata mshindi wa Miss Tanzania na kwa sasa tiketi zimepungua bei kama tulivyotangaza, viti vya kawaida itakuwa ni elfu 30, VIP 50,000 na VVIP ni 70,000, njoo tuandike historia mpya ya urembo Jumamosi hii pale JNCC,” alisema Basila.

Warembo wanaoshiriki shindano hilo ni pamoja na Nancy Matata, Pili Mtambalike, Amne Mkwanda , Queen Elizabeth Makune, Gladness Benson, Nelly Kazikazi, Osmunda Mbeyela, Sharon Headlam, Adilla Chigomello, Halima Kopwe.

Wengine ni Miriam Mmary, Zuhura Abdul, Teddy Mkenda, Hadija Rutunga, Azama Mashango, Florida  Mkungu, Linda Mhela, Ansila Mushi, Sandra Giovinazzo na Sheila Sheyla  Msira.

 

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*