MISS TANZANIA AYATAZAMA MASHINDANO YA DUNIA

NA JEREMIA ERNEST


MSHINDI wa shindano la Miss Tanzania 2018, Queen Elizabeth Makune, ametoa ahadi ya kufanya vizuri katika mashindano ya urembo ya dunia yanayotarajia kufanyika Novemba mwaka huu nchini China.

Queen Elizabeth, alilitwaa taji la Miss Tanzania kutoka kwa Diana Edward (Miss Tanzania 2016/17) juzi katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano ya Kimataifa wa Julius Nyerere, Posta Dar es Salaam baada ya kupenya kwenye mchuano mkali wa warembo 20 kutoka kanda mbalimbali nchini akifuatiwa na Nelly Kazikazi, Sandra Giovinazza kutoka Arusha.

Akizungumza na Papaso la Burudani baada ya ushindi huo, Elizabeth, alisema jukumu lililopo mbele yake ni kuhakikisha anaiwakilisha vyema nchi katika mashindano ya kimataifa, kutangaza utalii na kutwaa taji la urembo wa dunia.

“Niwatoe hofu Watanzania wenzangu, wategemee mabadiliko makubwa katika tasnia ya urembo hasa nitakapokwenda China lazima nirudi na taji, napokea ushauri kwa wadau ili kujiimarisha na mashindano hayo yaliyopo mbele yangu,” alisema Queen Elizabeth ambaye ni Miss Tanzania 2018 kutoka kanda ya Dar es Salaam.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*