Miss Tanzania aja na ‘Twenzetu Kutalii’

NA JEREMIA ERNEST

MISS Tanzania 2018, Queen Elizabeth Makune, anatarajiwa kuzindua kampeni ya kuhamasisha utalii wa ndani kupitia kampeni iliyopewa jina la ‘Twenzetu Kutalii’ katika hoteli ya Serena, Dar es Salaam, Agosti 30, mwaka huu.

Mrembo huyo ambaye ni balozi wa utalii wa ndani, ameliambia Papaso la Burudani kuwa baada ya kuzindua kampeni hiyo, utakuwa mwanzo wa kuratibu safari za utalii nchini.

“Kutakuwa na chakula cha jioni na burudani za asili kutoka makabila mbalimbali nchini, pia nitazindua kampeni hii ambayo ni mwanzo wa safari za kutalii zitakazohusisha vijana, wanawake, wanamume na jamii kwa ujumla,” alisema Queen.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*