Minziro akabidhiwa Alliance kuiua Simba

NA JESSCA NANGAWE

UONGOZI wa klabu ya Alliance, imemwajiri kocha Felix Minziro kwa lengo la kiufundisha timu yao inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Minziro aliyewahi kuifundisha timu ya JKT Ruvu kwa sasa JKT Tanzania, kocha msaidizi wa Yanga na Singida United ataanza kibarua chake kwa kucheza na Simba.

Mchezo huo  wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, umepangwa kucheza Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,  jijini Mwanza.

Akizungumza na BINGWA jana  Mwenyekiti  wa  klabu ya Alliance, Yusuph Budodi alisema kocha huyo tayari amekabidhiwa timu hiyo tangu Jumapili iliyopita.

“Ni kweli kwa sasa Minziro ni kocha wetu, ameanza kazi na mchezo wa kwanza atakaa kwenye benchi dhidi ya Simba.

Lengo la kumchukua kocha huyo ni uzoefu wake pamoja na uwezo wake  wa kuzikabili timu mbalimbali za Ligi Kuu Tanzania Bara,”alisema Budodi.

Alisema wanatambua mchezo ulio mbele yao ni mgumu, lakini watatumia vyema uwanja wao wa nyumbani wa Nyamagama kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

 Alliance inashika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 20, wakati Simba wakiwa kileleni kwa pointi 35.

@@@@


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*