MINAJ KUTOMFUNGULIA KESI CARDI B

NEW YORK, Marekani


MWANADADA Nicki Minaj, amesema hafikirii kumfungulia kesi mpinzani wake mkubwa katika muziki wa hip hop, Cardi B, baada ya tukio la hivi karibuni.
Taarifa ya siku chache zilizopita iliyotolewa na mtandao wa TMZ, ilidai kuwa wawili hao waligombana walipokutana katika hafla New York Fashion Week.
Katika tukio hilo, Cardi alimtupia kiatu mwenzake huyo lakini Nicki ametumia ukurasa wake wa Instagram kusema hana mpango wa kumpeleka mbele ya sheria.
“Nimepotezea mengi ya kipuuzi. Nilikuacha ‘unidis’, nilikuacha unisingizie uongo…nimepambana kufika hapa nilipo,” aliandika Nicki.
Awali, Nicki na Cardi waliwahi kukanusha mara kadhaa kuwa kwenye uhusiano mbaya lakini safari hii hawana cha kuficha tena kwani mambo ni moto.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*