MIL 500 KUJENGA JUMBA LA MAMA DIAMOND

NA KYALAA SEHEYE

IMEBAINIKA kuwa staa wa singo ya African Beauty Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ anamjengea jumba la kifahari mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’ maeneo ya Ununio, Dar es Salaam litakalogharimu shilingi milioni 500 kama zawadi.

Diamond amefikia maamuzi hayo baada ya kuona mama wengi waliotelekezwa na waume zao hushindwa kuwalea watoto na hatimaye hujikuta vijana wao wakiingia kwenye magenge ya uharifu.

Akizungumza na Papaso la Burudani mama mzazi wa Diamond alisema anamshukuru Mungu kwa zawadi hiyo anayopewa na mwanawe kwani ni heshima ambayo ataendelea kujivunia.

“Namshukuru mno Mungu, nilimlea Naseeb kwa shida baada ya kutelekezwa, hivyo akinipa zawadi yeyote sihitaji mtu aongee kwani anaamini kipindi kile angetokea Mkuu wa Mkoa kama Makonda basi leo hii mwanangu angekuwa na mafanikio zaidi kwani angepeta malezi ya pande zote mbili lakini nilimlea mwenyewe,” alisema Bi Sandra.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*