googleAds

Mgunda ataka usajili ‘bab kubwa’

ZAINAB IDDY

KOCHA wa timu ya Coastal Union ya jijini Tanga, Juma Mgunda, amesema kuwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara anahitaji kuwa na kikosi kipana na cha ushindani ili kuepukana na changamoto alizokutana nazo 2018/19.

Katika msimu huu uliofika tamati wiki hii, Coastal Union imemaliza ikiwa katika nafasi ya nane, ikiwa na alama 48 ilizozipata ndani ya mechi 38.

Akizungumza na BINGWA jana, Mgunda alisema msimu huu amefanikiwa kutimiza malengo ya kuibakiza timu katika ligi hiyo, lakini ujao mipango ya uongozi ni kuiwezesha kumaliza ndani ya nne bora.

“Nashukuru Mungu msimu huu nimetimiza malengo tuliyoyaweka na viongozi mara baada ya kupanda ligi kwa kuibakiza timu, lakini msimu unaokuja, lazima tuvuke malengo ya sasa.

“Katika ripoti yangu nitakayoikabidhi nitahitaji ufanyike usajili wa uhakika ambao utakuja kutupa kile wanachohitaji wadau wa Coastal Union,” alisema.

Aliongeza: “Sitokuwa tayari kuona ninaifundisha timu yenye wachezaji wengi wasio na viwango, nataka kila tutakayecheza naye, aondoke na kumbukumbu ya kupoteza mbele yetu.”


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*