MESSI AWAFUNIKA SALAH, RONALDO KIATU CHA DHAHABU

BARCELONA, Hispania

KWA lugha nyingine unaweza kusema wataisoma namba, baada ya straika wa Barcelona, Lionel Messi, kunyakua kiatu cha dhahabu Ulaya ikiwa ni mara ya tano kufanya hivyo.

Staa huyo wa timu ya Taifa ya Argentina, ametunukiwa tuzo hiyo baada ya msimu huu kufunga mabao 34 katika michuano ya Ligi Kuu ya Hispania, La   Liga yaliyoisaidia timu yake kutwaa taji lake la 25.

Messi alitokea benchi katika mchezo wa mwisho wa Barcelona uliopigwa juzi katika Uwanja wa Camp Nou dhidi ya Real Sociedad na kisha akatupia na hivyo kumfanya akabidhiwe tuzo hiyo ambayo aliwahi kuinyakua mwaka     2010, 2012 na 2013.

Idadi hiyo ilimfanya avuke    mabao 32 aliyokuwa nayo na kisha akamfunika Mohamed Salah, ambaye amefunga 32 tangu ajiunge na Liverpool na straika wa Tottenham, Harry Kane aliyeshika nafasi ya tatu akiwa na 30 aliyofunga katika michuano ya Ligi Kuu England.

Katika orodha hiyo, mshindi mara nne wa tuzo hiyo, Cristiano Ronaldo, alishika nafasi ya tisa akiwa na mabao 26 aliyoifungia Real Madrid katika michuano ya LaLiga.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*