Messi ampigia saluti Ronaldo

MADRID, Hispania

STRAIKA Lionel Messi, amempigia saluti mwenzake, Cristiano Ronaldo, kwa jitihada alizozifanya juzi ikiwa ni baada ya yeye kuonesha kiwango kizuri kilichoisaidia Barcelona kuichapa Lyon katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora.

Katika mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Nou Camp, Messi alifunga mabao mawili na kutengeneza mengine mawili yaliyoifanya Barca kuondoka na ushindi wa mabao 5-1, zikiwa ni wiki tatu baada ya mchezo wa kwanza timu hizo kushindwa kutambiana.

Ushindi huo ulikuja ikiwa ni baada ya juzi  hasimu wake, Ronaldo kutupia ‘hat-trick’ iliyoisaidia Juventus  kupata ushindi wa mabao  3-0  dhidi ya   Atletico Madrid  na hivyo kutinga robo fainali kwa jumla ya mabao 3-2.

Kufuatia hali hiyo, Messi, alikaririwa na gazeti la Marca baada ya mchezo huo na  Lyon akisema: “Kile ambacho  Cristiano Ronaldo  na Juventus walikifanya ni cha kuvutia.

“Nafikiri  Atletico Madrid ilikuwa ni timu ngumu, lakini  Ronaldo  alikuwa na usiku wa maajabu kwa kufunga mabao  matatu.”


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*