Messi amjia juu mwamuzi

RIO, Brazil 

STRAIKA wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi, amewatuhumu waamuzi kwa kuipendelea Brazil katika mchezo wa nusu fainali ya Copa America kwa kuwa wapinzani wao hao ni wenyeji wa michuano hiyo.

“Brazil haikuwa bora zaidi yetu, wamependelewa, tulipata penalti, lakini refa akapotezea, katika soka huwa inatokea kwa vile wao ni wenyeji, imetuathiri kwa upande wetu,” alisema Messi.

Brazil iliwachapa Argentina mabao 2-0 katika mchezo huo usiku wa kuamkia jana na hivyo kutinga fainali, ikisubiri mshindi kati ya Chile na Peru zilizotarajiwa kushuka dimbani leo alfajiri.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*