Meshack Salum amkingia kifua Rose Muhando

NA BRIGHER MASAKI

MWIMBAJI wa Gospo nchini, Meshack Salum, amesema kutokana na mazingira magumu aliyonayo mama wa muziki huo, Rose Muhando, jamii inapaswa kumwombea kwa Mungu na kuacha kumpa lawama.

Akizungumza na Papaso la Burudani jana, Meshack alisema Rose ameulea muziki wa Gospo, hivyo hapaswi kulaumiwa zaidi ya kuunganisha nguvu na kumwombea.

“Nampa pole sana, uzuri ni kwamba Mungu amempa neema ya kuendelea kuishi, hivyo niwashauri Watanzania kuwa wasimlaumu, bali wamwombee ili arudi katika hali yake kwa sababu mtu wa Mungu akirudi nyuma hatupaswi kufurahi,” alisema Meshack, ambaye yupo mbioni kukamilisha albamu yake.

Aidha, mlezi wa waimbaji wa Gospo nchini, Emmanuel  Mbasha, ameliambia Papaso la Burudani kuwa tayari amefanya mipango ya kutuma watu wakamchukue Rose Muhando nchini Kenya wamrudishe Tanzania, hivyo watu wasiwe na wasiwasi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*