googleAds

Mdogo wake Kanumba kuzikwa leo Dar

NA BEATRICE KAIZA

MWILI wa Seth Bosco ambaye ni mdogo wa nguli wa filamu nchini, marehemu Steven Kanumba, unatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam baada ya kufariki Dunia mwishoni mwa wiki.

Akizungumza na Papaso la Burudani jana, Athuman ambaye ni kaka wa Seth, alisema mdogo wake atazikwa eneo alilozikwa Kanumba.

“Shughuli za mazishi zitafanyika kesho (leo) katika makaburi ya Kinondoni, atazikwa saa 10 jioni pembeni ya kaburi la Kanumba,” alisema Athuman.

Miezi mitatu iliyopita, Seth ambaye pia ni mwigizaji, alipooza na baadaye kugundulika kuwa na uvimbe kwenye uti wa mgongo na baadaye akafanyiwa upasuaji ambao mpaka anafariki, alikuwa anaendelea na matibabu.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*