MCHUNGAJI ALIYENUSURIKA KIFO AMSHANGAZA DAVIDO

LAGOS, Nigeria


 

HIVI karibuni, ziliibuka taarifa kuwa mchungaji aitwaye Elijah ‘Mchungaji wa Miujiza’, alivamiwa na kupigwa risasi na watu wasiojulikana, tukio lililotokea katika Jimbo la Anambra.

Hata hivyo, kilichowashangaza wengi ni taarifa zilizoenea kwa kasi kuwa risasi hazikuweza kupenya kwenye mwili wa mtumishi huyo wa Mungu.

Jambo hilo limemshtua pia staa wa muziki, Davido, ambaye juzi alitumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, akisema alivyosikia alibaki na mshangao.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*