MCHEZAJI YANGA AKABIDHIWA TIMU KENYA

NA MWANDISHI WETU

ALIYEKUWA straika wa Yanga, John Baraza, amechaguliwa kuifundisha timu ya Sofapaka maarufu Batoto Ba Mungu, inayoshiriki Ligi Kuu Kenya.

Rais wa Sofapaka, Elly Kalekwa, alinukuliwa jijini Nairobi, Kenya, jana akisema Baraza anachukua nafasi ya Mganda Sam Ssimbwa aliyetangaza kujiuzulu mwishoni mwa wiki, baada ya timu yake kufungwa mabao 2-1 na Thika United katika mchezo wa ligi.

“Kocha amejiuzulu na msaidizi wake (John) Baraza amekabidhiwa mikoba,” alisema Rais wa Sofapaka.

Kalekwa anasema Ssimbwa anadai sababu ya kujiuzulu ni kuhujumiwa na wachezaji licha ya uongozi kumhakikishia sapoti.

Katika mchezo wake wa mwisho, Sofapaka walianza kupata bao la mapema lililofungwa na Kepha Aswani, lakini mabao ya Clement Mata na Edmond Adem aliyeingia kipindi cha pili yaliwapa Thika United ushindi wa kwanza msimu huu.

Ssimbwa ambaye ni kocha wa zamani wa timu za Express, KCCA na Soana zote za Uganda, anatarajiwa kutoa tamko leo.

Mbali na Baraza, mchezaji mwingine wa zamani wa Yanga, Benard Mwalala, anaifundisha timu ya Nzoia Sugar ambayo pia inashiriki Ligi Kuu Kenya.

Inaendelea………….. Jipatie nakala ya Gazeti la #BINGWA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*