googleAds

Mbonde aanza mazoezi mepesi

NA ASHA KIGUNDULA

BEKI wa zamani wa Simba, Salum Mbonde, ameanza mazoezi mepesi, baada ya kupona jeraha lililokuwa linamsumbua kuanzia msimu wa 2017/2018 wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na BINGWA jana, Mbonde alisema anafanya mazoezi chini ya uangalizi wa daktari wa tiba za michezo nchini, Gilbert Kigadya.

Alisema kwa sasa ana wiki mbili tangu aanze mazoezi mepesi huku akisubiria ripoti ya daktari ili aweze kujifua zaidi kujiandaa kwa usajili wa dirisha dogo la Ligi Kuu Bara.

Mbonde alisema ana uhakika wa kurudi uwanjani mzunguko wa pili Ligi Kuu Bara kwani ana uwezo wa kucheza soka katika klabu yoyote itakayomuhitaji dirisha dogo.

Beki huyo alisema anaamini atarudi na nguvu mpya hasa baada ya kukaa na kuangalia zaidi afya yake.

“Kwa sasa naendelea kuangalia afya yangu ila nina uhakika mzungumzo wa pili nikisajiliwa nitacheza maana mwili utakuwa umejengeka kimazoezi kwa sababu nitakuwa na muda mrefu wa kujiandaa,” alisema Mbonde.

Wachezaji wengine kutoka Mtibwa Sugar waliosajiliwa na Simba msimu wa 2017/18 ni Ally Shomari na Said Mohamed ‘Nduda’ ambaye amerejea katika timu yake hiyo ya zamani msimu huu.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*