Mbeya Kwanza kusajili wapya

NA GLORY MLAY

KOCHA wa Mbeya Kwanza inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, Maka Malwisi, amepanga kusajili wachezaji wapya kipindi kinachokuja cha dirisha dogo kitakachoanza Desemba 16, mwaka huu, hadi Januari 15, mwakani ili kuboresha kikosi chake.

Akizungumza na BINGWA juzi, Malwisi alisema malengo yake ni kusajili wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kuisaidia timu hiyo kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Malwisi alisema usajili  atakaoufanya utakuwa ni gumzo kwani anahitaji kupata wachezaji wazoefu kutoka nje ili kukimarisha kikosi hicho.

Alisema ligi msimu huu  ina upinzani mkali upinzani mkali kutokana na timu nyingi kuundwa na wachezaji wenye nguvu,  hivyo watajipanga kuhakikisha mzunguko ujao wanarudi kwa kishindo uwanjani.

“Tunahitaji kusajili wachezaji wenye uwezo wa kuhimili vishindo vya ligi, tunaomba sapoti ya wadau kuhakikisha tunafikia malengo yetu,” alisema Mwalwisi.

@@@@


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*