googleAds

MBELGIJI ABADILI GIA

NA HUSSEIN OMAR


 

BAADA ya kubanwa na kupata ushindi wa mabao 2-1 na African Lyon, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, ameamua kubadili gia angani na sasa amekuja na mbinu mpya zitakazomwezesha kupata mabao mengi zaidi.

Hatua ya Mbelgiji huyo inatokana na kikosi cha Simba kusheheni mastraika wakali wanaosifika kwa kufumania nyavu, lakini wakiwa wameshindwa kupata mabao mengi kulingana na ubora wao.

Lakini pia kasi ya watani wao wa jadi, Yanga katika kuzifumania nyavu, kumemfanya Aussems kuja na mkakati mpya wa ‘mvua’ ya mabao kwa kila timu watakayokutana nayo.

Akizungumza na BINGWA jana, Aussems alisema katika mazoezi ya leo yatakayofanyika Uwanja wa Boko Veterans, Dar es Salaam, atakuwa na kazi moja ya kuwafungia kazi mastraika wake katika suala zima la upachikaji wa mabao.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la BINGWA.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*