MBAO TIZI KUTWA MARA MBILI

NA MAREGES NYAMAKA


WAKATI mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania ikitarajiwa kuanza Desemba 27, mwaka huu, wachezaji wa Mbao wanatarajiwa kufanya mazoezi mara mbili kwa siku kujiandaa na ligi hiyo.

Akizungumza na BINGWA jana, Kocha wa timu hiyo, Etiemi Ndayiragije,  alisema  wanatarajia kuingia kambini Jumatatu ijayo kujiwinda na ligi hiyo.

Ndayiragije alisema anaamini wakianza mapema maandalizi wataweza kufanya vizuri katika mzunguko wa pili.

“Unajua maandalizi ya mapema yana faida nyingi, nimewaeleza vizuri wachezaji wangu namna ya kupata matokeo mazuri,” alisema Ndayiragije.

Alisema mzunguko wa pili wa ligi hiyo utakuwa mgumu kutokana na kila timu itahitaji kupata ushindi ili kuweza kuchukua ubingwa, lakini timu nyingine zikiepuka kushuka daraja.

Mbao inashika nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 16, huku Simba ikiwa kileleni kwa pointi 35.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*