googleAds

Mayanja aipania Coastal Union

NA GLORY MLAY

KOCHA wa KMC,  Jackson Mayanja, amesema kutokana na maandalizi waliyofanya anaamini wataibuka na ushindi dhidi ya  Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Akizungumza na BINGWA jana, Mayanja  alisema kikosi chake kipo  fiti,  baada ya kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo uliopita.

Mayanja alisema atahakikisha wanaondoka na pointi tatu dhidi ya Coastal Union, baada ya kuanza vibaya ligi hiyo kwa kufungwa na Azam bao 1-0.

Alisema anatarajia mchezo utakuwa mgumu kutokana na wapinzani wao watahitaji kushinda baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa na Polisi Tanzania bao 2-0.

 “Hatuna shaka tumejipanga na tunaamini tutaondoka na pointi tatu,  tumefanyia kazi mapungufu ambayo yalikuwa kwenye timu na tupo vizuri na tutashinda,” alisema Mayanja.

Alisema licha ya kuwa na majeruhi katika kikosi chake, lakini anaamini wachezaji wengine watafanya majukumu yao.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*