Mayanga asisitiza nidhamu Misri

NA ZAINAB IDDY

ALIYEWAHI kuwa kocha mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga, amesema nidhamu na kujituma ni vitu pekee vitakavyosaidia Stars kufanya vizuri katika Kombe la Afrika.

Taifa Stars ambao wanashiriki michuano hiyo kwa mara ya pili wapo Kundi C pamoja na Algeria, Senegal na Kenya.

Akizungumza na BINGWA, Mayanga alisema hivi sasa kikosi cha Stars kipo katika ubora tofauti na miaka ya nyuma hivyo kinaweza kufanya vizuri na kuwashangaza wengi.

“Stars ya sasa si ile ya kipindi kilichopita, kuna kila sababu ya kuleta changamoto mpya ndani ya AFCON, lakini jambo pekee litakaloibeba ni wachezaji kuwa na nidhamu pamoja na kujituma. Wanasema ukitaka kujua urefu wa kina cha maji lazima uingie kuyaoga, hivyo hata Stars inatakiwa kupambana wakijua wanacheza na timu kubwa na bora zaidi yao,” alisema.

Taifa Stars inashiriki mashindano ya AFCON mwaka huu baada ya kumaliza nafasi ya pili Kundi L wakiwafunga Uganda mabao 3-0 katika mchezo wa mwisho uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini  Dar es Salaam.

Kikosi cha Taifa Stars chini ya kocha mkuu, Emmanuel Okwi, kitaanza kutupa karata yake ya kwanza dhidi ya Senegal Juni 23 mwaka huu kabla ya kuwakabili Kenya na kumaliza mechi za makundi dhidi ya Algeria.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*