googleAds

MAVUGO, MO WAMKIMBIZA ATHANAS SIMBA

NA ZAINAB IDDY,

STRAIKA wa Simba, Pastory Athanas,  amekubali yaishe baada ya kuweka wazi nia yake ya kuvunja mkataba na klabu hiyo.

Meneja wa mchezaji huyo, Muhibu Kanu, ameliambia BINGWA kuwa  wamefikia uamuzi huo kutokana na kuwa na nafasi finyu aliyonayo mchezaji wake katika kikosi cha Wekundu hao.

“Si jambo zuri kuona mchezaji anakosa nafasi ya kucheza kisha ukaendelea kumuacha akae tu, baada ya ligi kuisha tutakaa na uongozi wa Simba ili kujua mustakabali wake na kama hatutaelewana itabidi aende akaangalie maisha mengine.

“Kimsingi hakuna mchezaji anayefurahia kukaa benchi, kila mmoja anataka kucheza ili kutoa mchango kwa timu yake lakini pia kuimarisha kiwango, kwa mantiki hiyo lazima tutafute namna ya kuokoa kipaji chake,” alisema Kanu.

Kocha wa Simba, Joseph Omog, amekuwa akipendelea zaidi kuwatumia mastraika Ibrahim Ajib, Ibrahim Mohamed na Laudit Mavugo hatua ambayo imekuwa ikisababisha maumivu kwa Athanas.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*