‘Mavituz’ ya Mane yampagawisha Fowler 

MERSEYSIDE, England

SADIO Mane ameisaidia Liverpool kuendelea kupaa angani katika soka la barani Ulaya, akishirikiana vyema na washambuliaji wenzake, Mohamed Salah na Roberto Firmino.

Moto wake wa kuzifumania nyavu hasa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, umemuibua nyota wa zamani wa Liverpool, Robbie Fowler ambaye alifunguka kwamba watu wengi hawampi sifa kama wanazopewa wenzake.

Fowler alisema anaamini Mane ni mchezaji asiyezungumzwa sana lakini anastahili kuwemo kwenye mijadala ya mchezaji bora wa mwaka, baada ya kuibeba Liverpool hadi nusu fainali ya UEFA.

Mane alifunga moja ya mabao manne yaliyofungwa na Liverpool dhidi ya Porto juzi, huku mengine yakiwekwa nyavuni na Salah, Firmino na Virgil van Dijk.

“Nakumbuka Mane alikuwa ni mchezaji mzuri sana mwaka jana, lakini wengi walikuwa wanamwangalia Salah. Siamini kama na mwaka huu anapotezewa licha ya kuonesha kiwango cha juu muda wote,” alisema.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*