MATATIZO YA MGONGO KUMZUIA PELE KWENDA URUSI

 RIO DE JENEIRO, Brazil

MICHUANO ya fainali za Kombe la Dunia mwaka huu, huenda zikawakosa nyota kadhaa wa zamani, baada ya staa wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil, Pele kuwa njiani kushindwa kufunga safari ya kwenda nchini Urusi kutokana na matatizo ya kiafya.

Matatizo hayo ya mgongo ambayo yanamkabili mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 77 ndiyo yaliyomfanya mwanzoni mwa wiki hii kushindwa kukabidhi Kombe la ubingwa  Campeonato Carioca kwa timu ya Botafogo, licha ya kuwa balozi wa mashindano hayo.

Kutokana na matatizo hayo, vyanzo  vya habari vilithibitisha juzi kwamba,vile vile kuna hali ya wasiwasi kama mshindi wa fainali hizo mara tatu ataweza kusafiri kwenda Urusi wakati wa fainali hizo za majira haya ya joto.

Hata hivyo, pamoja na Pele kukumbwa na matatizo tangu mwaka  2012, alipofanyiwa  upasuaji akishindwa kufunga safari hiyo, lakini bado atakuwa na nafasi ya kushiriki kutokana na kuwa ana mkataba wakuchambua mechi hizo na kituo kimoja cha televisheni Mbrazil.

Pele aliwahi kutwaa taji hilo mwaka  1958, 1962 na  1970 akiwa na  Brazil  na ndiye anayeongoza kwa upachikaji mabao akiwa na 77.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*