MASHABIKI BARCA WAMTIMUA PIQUE

CATALUNYA, Hispania


 

KWA kiwango kibovu alichokionesha katika mchezo wa Jumatano ya wiki hii dhidi ya Leganes, mashabiki wa Barcelona wamemtaka Gerard Pique kustaafu.

Ukiwa ni mwendelezo wa ‘maboko’ yake tangu kuanza kwa msimu huu, Pique alifanya kosa lililoipa Leganes bao la ushindi wakati mchezo huo ukiwa na matokeo ya sare ya bao 1-1.

Kabla ya kosa lake hilo, Pique, mwenye umri wa miaka 31, ambaye alianza kuichezea Barca mwaka 2008, wababe hao wa Catalunya walitangulizwa na bao la Philippe Coutinho (dk 21), lakini Nabil El Zhar alisawazisha.

Mmoja kati ya mashabiki wanaoamini uwezo wa Mhispania huyo umefikia mwisho, hivyo anatakiwa kustaafu, alitumia ukurasa wake wa twitter kuandika: “Hii ni mara ya pili Pique anatufanyia hivi, siwezi kuvumilia tena.”

              

 

 

 

 

 

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*