googleAds

Martial: Mfumo wa Solskjaer usipime

MANCHESTER, England

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Anthony Martial, amesema mfumo anaotumia kocha wao, Ole Gunnar Solskjaer, umemfanya kurudisha ubora wake.

Hivi karibuni, Martial alirudishiwa jezi yake ya zamani namba 9, ambayo aliwahi kuivaa kipindi anakipiga Monaco mwaka 2015.

“Ni jambo zuri kwa upande wetu, hata safu ya ulinzi ipo imara, inatufanya tucheze kwa uhuru. Mfumo mzuri pia umetusaidia kubadilishana nafasi, nina furaha kiukweli,” alisema Martial.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*