googleAds

Maproo hawa panga shingoni

NA WAANDISHI WETU

WAKATI wachezaji wa Simba, Deo Kanda na Francis Kahata wakifikiriwa kuondolewa au kubakizwa kikosini tayari Kamati ya usajili imewatia kitanzani nyota wake kutoka nchini Brazil baada ya kushindwa kufikia viwango walivyotaka.

Taarifa za ndani zilizonaswa na DIMBA Jumatano ni kuwa panga hilo litaanzia kwa Wabrazil ambapo usajili wa dirisha dogo wataenguliwa na kutafuta wachezaji wenye uwezo mkubwa kuisaidia timu hiyo.

Alisema, wameamua kuwaondoa Wabrazil kwa kushindwa kufanya vizuri katika michuano ya Kimataifa sambamba na Ligi Kuu ambayo inaendelea, lakini hata kwenye mechi za kirafiki kutokuonyesha mwanga.

Taaifa hiyo inaeleza kwamba WabraziL hao Gerson Fraga Vieira, Taroine da Silver na Wilker Henrique da Silver, walisajiliwa lengo likiwa ni kuonyesha uwezo mkubwa kuliko waliokuwepo, lakini mambo yamekuwa tofauti kabisa.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*