MAPOKEZI YA MARADONA MEXICO USIPIME

CULIACAN, Mexico


 

KOCHA wa zamani wa Argentina, Diego Maradona, juzi alipokelewa kama mfalme baada ya kuwasili  Mexico tayari kuanza kibarua cha Ukurugenzi wa Ufundi katika klabu ya  Dorados  ambayo inashiriki Ligi Daraja la Pili nchini humo.

Katika mapokezi hayo, baadhi ya mashabiki walikuwa wamebeba mabango ya kumtukuza kinara huyo wa soka wa zamani huku mengine yakionesha mashabiki hao wakimshukuru Mungu kwa ujio huo wa  Maradona.

“Karibu dhahabu ya Mungu. Asante Mungu. Asante Maradona,” lilieleza moja ya bango lililokuwa limebebwa na mmoja wa mashabiki waliojitokeza katika uwanja wa ndege mjini Culiacan.

Hata hivyo, akiwa amevaa mavazi  yote meusi na mkufu wa dhahabu na skafu iliyokuwa na rangi nyeupe na nyeusi,  Maradona hakuzungumza chochote na mashabiki waliojitokeza kumpokea.

Akiwa ameambatana na vigogo wa klabu hiyo na mwanasheria wake, Maradona alitumia muda mchache kuzungumza na waandishi wa habari na huku akiwa na shauku ya kukutana na wachezaji wake wapya.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*