Man Fongo, Snura wachengua Tigo Fiesta Moro

NA EMILIANA CHARLES (TUDARCO)

TAMASHA la Tigo Fiesta lililofanyika juzi katika Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro, lilikonga vilivyo nyoyo za mashabiki wa muziki, baada ya shoo ya nguvu iliyofanywa na wasanii waliopanda jukwaani, wakiwamo Man Fongo na Snura Mushi.

Wasanii lukuki waliopanda jukwaani kutumbuiza, walilitendea haki jukwaa, lakini Man Fongo na Snura waliwafanya mashabiki walipuke kwa kelele kutokana na aina ya muziki wao wa singeli pamoja na uchezaji.

Kwa sasa muziki huo wa singeli umeonekana kupendwa na watu wengi na kujipatia mashabiki lukuki na hiyo ndio sababu iliyowafanya Man Fongo na Snura kushangiliwa sana katika tamasha la Fiesta mbali na hapo wasanii hao walionekana kuimba sambamba na mashabiki wao tofauti na wenzao.

Mbali ya hao, wasanii wengine waliopanda jukwaani kwenye Tamasha la Tigo Fiesta ni pamoja na Weusi, Dully Sykes, Roma Mkatoliki, Ben Pol, Nandi, Maua  Sama, Fid  Q na wengineo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*