googleAds

Man City yamnasa Cancelo

MANCHESTER, EnglandĀ 

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu England, Manchester City, wameripotiwa kukamilisha usajili wa beki wa Juventus, Joao Concelo.

Katika usajili huo, Man City wamemtoa sadaka beki wao, Danilo, ambaye atajiunga na Juventus kama mabadilishano.

Imedaiwa Concelo amenaswa kwa pauni milioni 32 (sh bil. 89) na City walioipiku Bayern Munich ambao nao walikuwa wakimfukizia.

Imeelezwa kuwa Mkurugenzi wa Michezo wa Juventus, Fabio Paratici, amedai makubaliano ya pande zote mbili yapo katika hatua ya mwisho.

Cancelo, alifukuziwa vikali kwa muda mrefu na Pep Guardiola, ambaye amevutiwa na uwezo wake.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*