Man City wana sifa nyie

MANCHESTER, EnglandĀ 

KLABU ya Manchester City, ipo mbioni kumrejesha beki wao wa zamani, Angelino, kutoka PSV ili kukinukisha msimu ujao wa Ligi Kuu England.

Kwa sasa, Angelino mwenye umri wa miaka 22, yupo jijini Manchester, England ili kukamilisha uhamisho huo na huenda akatangazwa na klabu hiyo.

Ikumbukwe kuwa beki huyo, alicheza mechi zote msimu uliopita na kikosi cha PSV, huku wakishika nafasi ya pili mbele ya mabingwa wa Ligi Kuu Uholanzi, Ajax.

Kuna kipengele cha mchezaji huyo kinachoeleza kuwa Man City wana uwezo wa kamnunua tena kwa pauni milioni 5 (sh bil.14), kama sehemu ya masharti walipoamua kumpiga bei.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*