MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU RONALDINHO

ANAITWA Ronaldo de Assis Moreira, ila mashabiki wa soka ulimwenguni kote wanamfahamu kwa jina Ronaldinho ‘Gaucho’.

Hivi karibuni, staa huyo wa zamani wa PSG, Barcelona na AC Milan, alitangaza kutundika daluga akiwa na umri wa miaka 37.

Mbali na mafanikio mengine, Ronaldinho anastaafu akiwa ameshinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na tuzo ya Ballon d’Or katika maisha yake ya soka.

Nyota huyo alionekana uwanjani kwa mara ya mwisho mwaka 2015 akiwa anaichezea Fluminense ya Ligi Kuu ya Brazil.

Haya ni mambo 10 yanayomhusu Ronaldinho, ambaye mashabiki wa soka watamkumbuka kwa ufundi wake wa kuchezea mpira, chenga na mabao ya ‘kideo’.

  1. Jina lake lilianza kuwa gumzo kwenye vyombo vya habari nchini Brazil baada ya kufunga mabao yote wakati timu yake ya mchangani iliposhinda mabao 23–0. Kipindi hicho alikuwa na umri wa miaka 13.
  2. Ronaldinho, ambaye ni baba wa mtoto mmoja aliyezaa na dansa wa Brazil, Janaina Mendes, ana uraia wa Hispania alioupata rasmi mwaka 2007, akiwa staa wa Barcelona, iliyokuwa chini ya Frank Rijkaard.
  3. Mwaka 2001, Arsenal walikaribia kumchukua, lakini kilichokwamisha ni kibali cha kazi nchini England. Alitakiwa kwenda kucheza Scotland kwa mkopo, lakini yakazuka majanga ya kuhusishwa na uhuni wa kughushi hati ya kusafiria.
  4. Barcelona walimsajili ili kuchukua nafasi ya kiungo David Beckham, ambaye aliwakataa na kwenda Real Madrid. Barca walitoa euro milioni 30 ili kuipoteza Man United, ambayo pia ilikuwa ikimfukuzia.
  5. Ronaldinho na Diego Maradona ndio wachezaji pekee wa Barcelona waliowahi kushangiliwa na mashabiki wa Real Madrid katika Uwanja wa Santiago Bernabeu. Ronaldinho alikutana na shangwe kutoka kwa mashabiki wa wapinzani hao katika mchezo wa Clasico mwaka 2005……………..
  6. kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya BINGWA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*