googleAds

Makocha wasuasua kuomba ajira KMC

NA ZAINAB IDDY

IKIWA ni miezi miwili tangu kuondoka kwa Jackson Mayanga KMC, ni makocha saba pekee ndiyo walioomba ajira ya kukinoa kikosi hicho.

KMC ilitangaza rasmi nafasi ya ajira ya Desemba, mwaka jana na kati ya makocha walioomba kukinoa kikosi hicho, watatu ni wageni.

Akizungumza na BINGWA jana, Kaimu Katibu Mkuu wa KMC, Walter Harrison, alisema hadi kufika jana jioni, walikuwa wamepokea barua saba za maombi.

“Sijajua kama kuna maombi mengine yameingia leo(jana), barua za tangu jana(juzi) nilizopokea ni saba saba kati yao kutoka nje ya Tanzania ni watatu tu.

“Baada ya kukamilika kwa zoezi hili, Kamati ya Utendaji ya KMC itakutana na kuzipitia kisha kuangalia kama atakayetufaa na kuzungumza nae kuhusu mkataba

“Tunaamini mchakato huu, tutampata kocha bora atakayekidhi vigezo na kuweza kutuletea mafanikio katika michuano tunayoshiriki,” alisema Harrison.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*