googleAds

Makocha wa Liverpool washusha neema Bongo

Elizabeth Joachim,Dar es Salaam

Makocha wawili, Anthony Godfrey na Dave Rogers, waliowahi kufundisha timu za vijana wametua kwa ajili ya mafunzo ya soka kwa vijana wadogo nchini.

Makocha hao wameletwa na kituo cha 7 Elite Academy kutoka Marekani, chini ya raisi wake Reggie Wilson, ambapo wanashirikiana na watanzania wengine, akiwemo mchezaji wa zamani wa Simba na Yanga, Amri Kiemba.

Akieleza lengo la kuja nchini leo Aprili 27 Jijini Dar es salaam, Wilson amesema “Tumeichagua Tanzania kwa kuwa ni nchi yenye vipaji vingi ambavyo vilikosa usimamizi, hivyo tunaamini endapo shirikisho litatupa sapoti, kwa pamoja tutainua soka la nchi.

Wilson amesema watatoa mafunzo kwa watoto wa umri chini ya miaka 17, lakini pia watakuwa na kozi za makocha kwa kuwa wanajua hakuna soka bora pasipo na walimu bora,”

Naye Kocha Anthony amesema: “Nilikaa kwenye Academy ya Liverpool kwa zaidi ya miaka 12, hivyo naelewa mfumo wa soka la Vijana na ndiyo maana tumekuja hapa kwa lengo la kwapa mafunzo vijana ili waje kuwa wanasoka wa dunia,”.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*