googleAds

Makarova amnyoosha Konta

download (5)

TORONTO, Canada

NYOTA wa tenisi, Johanna Konta ameshindwa kufurukuta mbele ya Mrusi, Ekaterina Makarova katika raundi ya pili baada ya kuchapwa kwa seti 5-7, 7-6 (7-4) na 6-3 kwenye michuano ya Rogers Cup.

Konta, alicheza mechi yake ya kwanza tangu alipopoteza kwenye nusu fainali ya Wimbledon, dhidi ya Venus Williams.

Muingereza huyo mwenye mwenye umri wa miaka 26, aliweza kuongoza kwa seti 7-5 na 5-2 lakini seti ya pili ilimshinda na hapo ndipo aliponyooshwa.

Huo ni ushindi wao saba mfululizo kwa Makarova, 29, ambaye anakamata nafasi ya 42.

Aidha, Mrusi huyo alitegemewa kuonesha upinzani mkali kwa Konta, lakini haikuwa rahisi kwake licha ya kumshinda.

Kutokana na ushindi huo, Makarova atakutana na Lucie Safarova kwenye raundi ya tatu ya michuano hiyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*