Mahadhi arejea dimbani, Kabwili majanga

NA WINFRIDA MTOI

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Juma Mahadhi, anatarajia kuonekana uwanjani katika mechi zijazo baada ya kupona majeraha ya muda mrefu yaliyokuwa yakimsumbua.

Mahadhi amekaa nje ya uwanja zaidi ya mwaka mmoja baada ya kutonesha goti katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger mwaka jana na kumfanya afanyiwe upasuaji.

Akizungumza na BINGWA jana, daktari wa Yanga, Sheky Mngazija, alithitisha mchezaji kupona na anaweza kurejea uwanjani muda wowote.

“Mahadhi anaweza kurejea katika majukumu yake kwa sasa, hakuna tatizo lolote, tunamwachia mwalimu ndiye mwenye maamuzi ya kumtumia,” alisema.

Katika hatua nyingine, Mgazija, alisema majeruhi aliyepo kwa sasa kikosini kwao ni Ramadhani Kabwili ambaye amepata ajali ya pikipiki na kushonwa nyuzi nane kwenye paji la uso.

Alisema wanaendelea kumfatilia kwa karibu apate matibabu mazuri ili aweze kupona haraka na  kurejea uwanjani.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*