Madee amtolea povu Pogba

NA GRAY PAUL (TUDARCO)

RAPA kutoka Tip Top Connection, Hamad Ally ‘Madee’, jana aliwashangaza mashabiki zake mara baada ya kutoa maneno yaliyozua mjadala kuhusu mchezaji wa Manchester United, Paul Pogba.

Madee alitoa maneno hayo baada ya Manchester United kupoteza mchezo wa tatu mfululizo na kiungo huyo ghali aliyevunja rekodi ya usajili wa pauni milioni 89 akitokea Juventus na kuandika maneno ya kuwatia moyo mashabiki wa klabu hiyo kupitia Instagram.

“Utaweza wapi wewe rudisha mapene ya watu, we mtu gani hufungi, mbona yule Xhaka kafunga jana,” aliandika Madee kwenye ukurasa wa Pogba na kuzua mjadala mzito mtandaoni.

Papaso la Burudani lilipomtafuta Madee, alisema alitaka kuonyesha kuwa lugha ya Kiswahili inaweza kuandikwa kwenye kurasa za mtu yeyote maarufu kama wanavyofanya mashabiki wa mataifa mengine wanaotumia lugha za mataifa yao.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*