LWANDAMINA ATAKA VIWANJA VITATU YANGA

NA SALMA MPELI

KOCHA mpya wa Yanga, George Lwandamina, ametaka wachezaji wake kufanya mazoezi katika viwanja vitatu tofauti kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Yanga wanaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana Dar es Salaam, huku Lwandamina akihitaji uwanja mwingine ili waweze kupata mazoezi kwa kucheza viwanja vyenye viwango tofauti.

Habari zilizopatikana jana kutoka ndani ya klabu hiyo, zilieleza kwamba Lwandamina ameomba kufanya mazoezi kwenye viwanja vitatu tofauti ili kuzoea mazingira ya viwanja wa mikoani.

Mtoa habari wetu alisema, Lwandamina ametaka wafanye mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani, Gymkhana ambapo walifanya jana jioni na Chuo cha Polisi ambao walianzia mazoezi yao  Jumatatu wiki hii.

Alisema baada ya Gymkhana wataangalia uwanja mwingine watakaotumia kufanyia mazoezi hayo kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili  Ligi Kuu Bara.

“Leo (jana) asubuhi hatujafanya mazoezi,  lakini jioni tutafanya kwenye Uwanja wa Gymkhana na baada ya hapo tutatafuta uwanja mwingine kwani kocha ametaka kupata viwanja tofauti ili kuona mazingira kwa kulinganisha na viwanja vya mikoani,” alisema mtoa habari wetu.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*