LULU DIVA AFUNGUKA KUTENGENEZA NGOZI A.KUSINI

NA ESTHER GEORGE


 

MREMBO anayefanya vizuri katika Bongo Fleva na wimbo wa Ona, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’, amesema sababu iliyomfanya atengeneze ngozi yake Afrika Kusini ni kuipa hali ya mvuto zaidi.

Lulu Diva ameliambia Papaso la Burudani kwamba, anapenda masuala ya urembo na yupo tayari kufanya chochote ili aendelee kuwa mrembo japo hayupo tayari kutaja gharama aliyoitumia kutengeneza ngozi yake.

“Niliamua kutengeneza ngozi yangu nchini Afrika Kusini ili iwe na mwonekano wa urembo na yenye mvuto zaidi, napenda urembo nipo tayari kufanya kila ninaloweza ili niwe mrembo,” alisema Lulu Diva.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*