LULU ATOA MSAADA AKIWA JELA

NA MEMORISE RICHARD

IKIWA ni miezi mine imepita toka mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, ahukumiwe kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kumuua msanii Steven Kanumba bila kukusudia, mrembo huyo ametoa msaada wa taulo za kike kwa ajili ya kuwasaidia wasichana, katika kampeni inayoendeshwa na kituo cha runinga EATV.

Akizungumza na waandishi wa habari jana maeneno ya Mikocheni Dar es Salaam, Dr Cheni alisema taulo hizo za kike amepewa na Lulu ambaye yupo jela kwa kuwa anawapenda na anataka wawe huru hata wanapokuwa kwenye ‘ada’ zao za mwezi.

“Nimekuwa nikimtembelea mara kadhaa na kumjulia hali na yeye ameomba ashiriki kwenye kampeni hii ingawaje hayupo, yupo jela na zaidi ameniambia niwaambie mabinti wa kitanzania wasitate tamaa  katika harakati za kutimiza malengo yao na Mungu atawasaidia,” alisema Dr Cheni.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*