LULU AIBUKA MTANDAONI KUMPONGEZA MCHUMBA WAKE

NA CHRISTOPHER MSEKENA


 

BAADA ya kupata msamaha wa Rais John Magufuli na kuanza kutumikia kifungo cha nje, staa wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, ameibuka katika mtandao wa Instagram na kumtakia heri ya kuzaliwa mchumba wake, Francis Ciza maarufu kama Rdj Majizzo.

Lulu ambaye anatarajia kumaliza kifungo chake cha nje, alijiweka mbali na mtandao huo wa picha toka Oktoba 22 mwaka jana, aliweka picha ya mchumba wake na kuandika maneno ya kumtakia heri ya kumbukizi ya kuzaliwa.

“Mpenzi, rafiki wa dhati, mshirika wa biashara na mtu ninayekulalia begani ninapolia, asante kwa kunionyesha upendo wa Agape, baraka zikufikie siku zote za maisha yako, nakutakia heri ya kuzaliwa kwake, nakupenda,” alisema Lulu ambaye kifungo chake kilikuja baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia mwigizaji, Steven Kanumba.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*