googleAds

Lukaku aonyesha cheche Inter Milan

MILAN, Italia

Mshambuliaji mpya wa Inter Milan, Romelu Lukaku, amefunga mabao manne peke yake katika mechi yake ya kwanza akiwa na kikosi hicho dhidi ya Virtus Bergamoya Ligi Daraja la Nne, wikiendi iliyopita.

Lukaku alijiunga na Inter dakika za mwisho, kabla ya dirisha la usajili halijafungwa, kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 74 (sh bil.204) akitokea Manchester United.

Inter iliichapa Bergamo mabao 8-0, katika mechi ya kirafiki, ukiwa ni mchezo wa kujiandaa na msimu mpya.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*