LOW ALIA KUKIMBIWA NA OZIL

LONDON, England


 

KOCHA wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low, juzi alitembelea Uwanja wa Emirates, lakini staa wake wa zamani anayeichezea Arsenal, Mesut Ozil, hakufika.

Low alifika Emirates, ambako aliweza kuzungumza na Mjerumani mwenzake ambaye kwa sasa ni mkuu wa ‘academy’ ya Arsenal, Per Mertesacker.

Tangu Ozil alipostaafu soka la kimataifa kwa madai ya ubaguzi, Low amekuwa akidai kuwa Ozil hataki kukutana naye na uhusiano wao umekufa.

“Mesut hakuwa mazoezini na tunakubali kuwa hakutaka kuzungumza na sisi kwa muda huo. Sijajua sababu,” alisema Low.

“Binafsi nimesikitishwa na nitajaribu kutafuta nafasi ya kuzungumza naye, kwa sababu bado yupo karibu na moyo wangu,” alisema Low.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*