Lipuli yawaita Yanga mezani

NA WINFRIDA MTOI

UONGOZI wa Lipuli FC, umesema hautamzuia mchezaji wao anayetakiwa na timu yoyote katika kipindi cha dirisha dogo la usajili unaoanza mwezi huu.

Kauli hiyo Lipuli imetokana na tetesi kuwa klabu ya Yanga iko mbioni kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo, Daruesh Saliboko.

Akizungumza na BINGWA jana, Mwenyekiti wa Lipuli FC, Ayoub Kihwelo, alisema kama kuna timu inahitaji mchezaji kutoka kwao, ifuate taratibu zinazotakiwa.

Alisema wachezaji wao bado wana mikataba, lakini wanajua soka ni biashara siku hizi, hivyo hakuna haja ya kumzuia mchezaji kuondoka endapo atapata sehemu inayomlipa vizuri.

“Taarifa za wachezaji wetu kutakiwa na Yanga au Simba, tunazisikia tu, lakini hakuna klabu iliyoleta ofa na kama ipo tunaikaribisha mezani,”alisema Kihwelo. Tofauti na Saliboko, nyota mwingine wa Lipuli anayefukuziwa na timu mbalimbali ni Paul Nonga ambaye anachuana na Meddie Kagere katika ufungaji


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*