Lindelof kupewa donge nono

MANCHESTER, England

KLABU ya Manchester United ipo tayari kumpa mshahara mnono beki wake tegemeo, Victor Lindelof, kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail.

Imeelezwa kuwa Lindelof atakuwa akilipwa pauni 150,000 kwa wiki na kuiziba mdomo Barcelona iliyokuwa ikimnyatia beki huyo.

Lindelof na Harry Maguire walikuwa na kiwango kizuri katika mechi ya kwanza ya ufunguzi wa Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea wikiendi iliyopita ambayo United ilishinda mabao 4-0.

Hata hivyo, beki huyo mwenye umri wa miaka 25, Lindelof, amebakiza miaka miwili katika mkataba wake.

Itakumbukwa kuwa Lindelof alijiunga na Man United mwaka juzi kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 30 (zaidi ya Sh bil. 83 za Tanzania) akitokea Benfica.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*