Ligi ya vijana ngazi ya Taifa kuanza Juni

NA MWANDISHI WETU

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limesema Ligi ya Vijana Ngazi ya Taifa chini ya umri wa miaka 15 na 17 itaanza Juni mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa jana kwenye vyombo vya habari na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Ndimbo, kwa sasa ligi  hiyo inaendelea ngazi ya wilaya.

Taarifa hiyo ilisema  imeanzisha kwa juhudi za  TFF katika harakati za kuendelea kuwekeza katika soka la vijana.

Ilisema ligi ya vijana ngazi ya wilaya inatarajia kumalizika mwishoni mwa Aprili, baadaye kuendelea ngazi ya mkoa Mei, mwaka huu.

Taarifa hiyo ilisema TFF inaendelea kuwekeza katika soka la vijana ambako ni msingi wa maendeleo ya soka.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*