googleAds

Ligi Daraja la Kwanza netiboli kufanyika Dodoma

HELLEN GERALD (TUDARCo)

Ligi Daraja la Kwanza ya netiboli, imepangwa kufanyika jijini Dodoma, ikishirikisha timu 19 za wanawake na wanaume.

Daraja la Kwanza ya netiboli, imepangwa kufanyika jijini Dodoma, ikishirikisha timu 19 za wanawake na wanaume.

Akizungumza na BINGWA juzi, Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta),  Judith Ilunda, alisema ligi hiyo itaanza mwishoni mwa mwezi huu.

“Tumejipanga vizuri na tunatarajia mashindano ya mwaka huu kuwa na msisimko mkubwa kutokana na maandalizi bora yaliyofanywa timu shiriki,” alisema Judith.

Katika hatua nyingine, Judith alisema Ligi Daraja la Pili itaanza  Novemba, mwaka huu, mkoani Morogoro, ikishirikisha timu 20 kutoka Tanzania Bara.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*