LEBRON AKIPA KISOGO KICHAPO NBA

LOS ANGELES, Marekani


 

STAA LeBron James, haoni sababu ya mashabiki wa Cleveland Cavaliers kuwa na wasiwasi kwa kichapo walichokipata kutoka kwa Boston Celtics, mchezo wa Ligi Kuu ya Kikapu ya Marekani (NBA) uliochezwa juzi.

Celtics walikuwa mwiba mchungu kwa Jumapili, wakiibuka na ushindi wa pointi 108-83 dhidi ya Cavaliers.

Licha ya timu yake kupoteza mechi hiyo ya Ukanda wa Magharibi, James aliweza kuondoka dimbani akiwa ametupia pointi 15.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*