googleAds

LAMPARD KUIBANIA CHELSEA KOMBE LA CARABAO?

LONDON, England

RATIBA ya mechi za mzunguko wa nne Kombe la Carabao imetangazwa na timu ya Derby County inayonolewa na Frank Lampard, itachuana na Chelsea.

Itakuwa ni mara ya kwanza kwa Lampard kurudi Stamford Bridge kama kocha wa timu nyingine dhidi ya Chelsea ambayo aliwahi kuichezea miaka ya nyuma.

Derby ilifanikiwa kutinga katika hatua hiyo baada ya kuing’oa Manchester United kwa mikwaju ya penalti wiki iliyopita, ambapo ilikuwa ni vita kati ya Lampard na kocha wake wa zamani, Jose Mourinho.

Lakini, katika mechi za mzunguko ujao Lampard ataiongoza timu yake hiyo dhidi ya vigogo wa Ligi Kuu England, Chelsea.

Je, ataibania timu yake hiyo ya zamani, hiyo siku ya Oktoba 29?

Mechi nyingine ni hizi hapa:

West Ham v Tottenham

Man City v Fulham

Arsenal v Blackpool


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*