Laizer awakutanisha Otile Brown, Vera Sidika

NA CHRISTOPHER MSEKENA

MTAYARISHAJI nyota wa muziki nchini, Laizer Classic, amefanikiwa kuwakutanisha kwa mara ya kwanza toka waachane mastaa kutoka Kenya waliowahi kuwa wapenzi, Otile Brown na mrembo Vera Sidika.

Laizer, ambaye amepata dili la kuwa mmoja ya watayarishaji wa muziki  watakaotengeneza nyimbo za wasanii watakaoshiriki msimu mpya wa Coke Studio jijini Nairobi, Kenya, aliweza kufanya kazi na wasanii hao japo hakutaka kuweka wazi kama ni kolabo au kila mtu na wimbo wake.

“Nilipiga picha na Vera na Otile baada ya kurekodi, tumefanikiwa kufanya kitu ingawa ni mapema sana kuzungumzia hizo projekti,” alisema Laizer.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*